Gisi ya kuzuwia magonjwa ya kuambukia
Magonjwa ya kuambukia inaweza kusababisha vinyume kubwa katika maisha yetu. Angalia mbinu ya kuzuwia maambukizi ya magonjwa ya kuambukia katika maeneo ya mikutano.
IPAC ni nini?
Infection prevention and control (IPAC) ni mbinu inayo tumia ushahidi inayo lenga kuvunja uhusiano katika njia ya kusambalaza maambukizi na kuzuwia watu kuingia kwenye hatari kutokana na maambukizi inayo sababishwa na mikrobe ambayo inaweza kuepukwa.
Njia za kuvunja hali ya kusambalaza maambukizi ni pamoja na:
- Kunawa mikono mara kwa mara na kufunika mdomo wakati unakohola na kupiga chafya
- Kuhakikisha unapata chanjo inayo faa
- Kubakia nyumbani wakati unakuwa mgonjwa
- Kusafisha na kutumia dawa ya kuuwa mikrobe katika mazingira yako
- Kuweka chakula vizuri
- Kutumia muzuri chombo ya kuwekea uchafu
Usafi wa mikono
Mikono ni njia ya kwanza ya kusambalaza mikrobe. Kunawa mikono yako mara kwa mara imeonekana kupunguza kwa kiasi kikubwa maambukizi ya homa na COVID-19, mafua ("mafua") na maambukizi zingine. Ni vizuri kuweka makucha za mfupi na kuzingatia ma bijoux zenye unavala, kwa sababu likucha ya mrefu, makucha za kuongeza na ma bijoux ni njia kubwa ya kujificha kwa mikrobe.
Sabuni na Maji: Mbinu 4 ya kunawa mikono
Kutumia désinfectant ao papier ya kupanguza mikono
Kunawa mikono na sabuni na maji ni njia bora ya kutowa mikrobe mara mingi.
Kama sabuni na maji havipatikani kwa urahisi, unaweza kutumia désinfectant ya mikono iliyo tengenezwa na alcool yenye kiasi isiyo chini ya 60% ya alcool. Unaweza kujua ya kama désinfectant ya mikono ina kiasi isiyo chini ya 60% ya alcool kwa kusoma étiquette yake.
Kutumia gants, barakoa na Vifaa vya kujikinga vya Kibinafsi (EPI)
Barakoa na gants ni mifano ya Vifaa vya Kujikinga vya Kibinafsi (EPI), ambavyo vinakinga mwili yako zidi ya mikrobe.
Kuvala barakoa inasaidia kuwalinda wengine kwa kuzuwia mikrobe isisambalane kwa wengine.
Barakoa ya sura inaweza kusaidia kuzuwia mikrobe kutawanyika mu hewa na kwenye fasi. Ni muhimu kunawa mikono yako mbele na kisha kuvala barakoa. Hakikisha inafunika muzuri pua yako, mdomo na kidevu.
Tumia gants wakati wa kugusa vitu ao fasi ambazo zinaweza kuwa zimeambukizwa na mikrobe. Gants zinapashwa kutoshwa mara moja kisha kugusa fasi ya buchafu na kisha kunawa mikono kwa kutumia sabuni na maji.
Mbinu 4 za kukusaidia kujua mafaa ya kuvala barakoa
Pulizia dawa na safisha fasi ya kazi ya VAW na I&I
Kusafisha kila siku fasi zinazo guswa sana ndani ya machumba na fasi za kuishi za kawaida ni muhimu kwa kupambana na usambazaji wa mikrobe na kupunguza hatari ya maambukizi. Sisi wote tunaweza kuchangia ili kusaidia kuweka mazingira yetu safi.
Kama fasi fulani inajaa buchafu, safisha kwanza fasi hiyo kwa kutumia kitambala ya kulowana na sabuni. Kisha unaweza kutumia desinfectant (chupa ao kipanguzisho) kupanguza fasi hiyo muzuri. Angalia maagizo ya mtengenezaji kwenye chupa (vipanguzisho) kwa utunzaji salama na unao faa. Subiri fasi hiyo kukauka kwa hewa na usisahau kunawa mikono yako wakati unamaliza!






