Eneo ya Watoto

Karibu kwenye fasi iliyo tengenezwa kwa ajili yako tu kujifunza kuhusu magonjwa hatari ya kuambukia.

An illustration of a variety of different colour virus and germ shapes

Kutokana na COVID-19, sisi wote tunazungumuzia magonjwa hizi siku. Kwa hivyo ugonjwa wa kuambukia ni nini?

Magonjwa ya kuambukia, kama COVID-19, inasababishwa na viumbe kama bakteria, virusi, ao shampinyo. Sisi wote tunaishi na viumbe hivi vidogo inje na ndani ya mwili yetu. Kuna wakati viumbe hivi vinasaidia, kama vile bakteria ndani ya butumbutumbu yetu zinatusaidia ku digérer chakula. Lakini kuna zingine ambazo zinaweza kuwa na hatari kwetu na kusababisha magonjwa kama vile VIH, homa ya kawaida, malaria na kazalika.

youtube-video-thumbnail

Ukweli 3 wa kufurahisha

Blue virus icon

Hepatite B ndio Ugonjwa wa kawaida zaidi wa kuambukia

Hepatite B, ambayo inasababishwa na virusi, inaambukia watu bilioni 2 duniani kote. Hepatite B inaweza kusambalana kutoka kwa mtu mpaka mwengine kupitia damu, kiungo cha uzazi ao vimajimaji ingine vya mwili. Inashambulia maini na inaweza kuzuiliwa kwa chanjo.

Green bacteria icon

Edward Jenner alitengeneza chanjo ya kwanza mwaka 1796!

Daktari wa Uingereza, Edward Jenner, alitumia virusi zaifu ya ngombe (varioile de vache) ili kusaidia kutengeneza kinga zidi ya petite variole. Alipata wazo hiyi alipo gundua kwamba wajakazi wa kukamua maziwa na wachuruzi wa maziwa walikuwa na kinga zidi ya

petite variole.

Orange bacteria worms icon

Dalili za ugonjwa zinaweza kusababishwa na mfumo wako wa kinga kufanya kazi yake

Unapo pata homa ao mafua, mwili yako inakulinda zidi ya ugonjwa huo. Dalili hizi zinamaanisha kwamba uko na mfumo bora wa kinga! Unaweza kupata dalili hizi unapo chanjwa pia - na tena ni mfumo wako wa kinga njo unafanya kazi yake kwa kujifunza gisi ya kupiganisha na ugonjwa huo.

Pata Rangi

Download three unique disease colouring pages and make your own infectious disease!

kids-colouring

Njia 5 za kuwa na usalama na afya

An illustration of washing hands

Nawa mikono yako

Kuna viumbe vingi vidogo na mikrobes tunazo beba  kila mahali. Nawa mikono yako kwa sabuni na maji kwa angalau sekunde 20 ili kuepuka kugonjwa kutokana na mikrobes za kuambukiza. Sirita mbele na nyuma ya kila mkono na katikati ya vidole. Hesabia muda kwa kuimba wimbo wa "Joyeux Anniversaire" mara pili.

An illustration of washing hands
An illustration of a house with germs and virus symbols inside of it

Wakati uko mgonjwa, bakia nyumbani

Kama uko na dalili zozote za ugonjwa wa kuambukia, kama homa, homa ya mafua, kikohozi, na kazalika, bakia nyumbani. Unaweza kusambalaza mikrobe unapo karibiana na wengine, kwa hivyo kwa kubakia nyumbani siyo tu unapumuzika lakini unakinga wengine!

An illustration of a house with germs and virus symbols inside of it
An illustration of three plates and cutlery

Kula milo 3 iliyo pangwa muzuri kwa siku

Unapashwa kula milo 3 kila siku zenye lisho (nutriments) bora. Hiyi itasaidia seli zote katika mwili yako kudumu na afya, ikiwemo seli zako za kinga. Seli za kinga zenye afya ni muhimu sana kukulinda na magonjwa ya kuambukia.

An illustration of three plates and cutlery
An illustration of a glass of water

Kunywa maji mingi!

Unapashwa kunywa vikombe 8 vya maji kila siku. Maji inasaidia kusafirisha lisho muhimu kati ya seli za mwil yetu. Hiyi ni muhimu sana kwa sababu inatusaidia kutowa uchafu mwilini mwetu na kubakia safi ndani ya mwili yetu! Unapashwa kunywa maji iliyo chemushwa ao iliyo chujwa unapo weza kufanya hivo ili kuepuka kunywa buchafu.

An illustration of a glass of water
An illustration of water drops washing an apple and a pepper

Safisha chakula yako yote kwa maji inayo tiririka mbele ya kupiga ao kula

Sawa vile mikono yako, chakula yako inaweza pia kubeba viumbe hatari. Mbele ya kula nyama yako, kuku, samaki, matunda ao mboga mboga, unapashwa kuzinawa muzuri kwa kutumia maji ya bomba. Hiyi inaweza kusaidia kutowa mikrobe kwenye chakula yako mbele ya kupiga ao kula.

An illustration of water drops washing an apple and a pepper
An illustration of a variety of different colour virus and germ shapes

How to learn more

Explore these other helpful links to learn more about infectious diseases and how to protect yourself!

Scroll To Top